Baba yake Bwana Mwamburi, alifungua mlango wa nyumba yao ya msonge. Alikuwa amekasirika sana. “Ruto! Ruto rudi hapa! Nilikwambia leo huendi shuleni. Umesikia,” Baba yake akasema. “Kwa nini baba? Ninataka kusoma. Ninataka niwe daktari. Mwalimu alisema, nikitia bidii masomoni nitakuwa daktari.”